Serikali imeiagiza Menejimenti ya Ranchi za Taifa nchini (NARCO) kuchukua hatua sitahiki kwa wafugaji waliokiuka sheria ,kanuni ,taratibu, miongozo na masharti ya mikataba yao ya kuendesha shughuli zao za ufugaji kwenye  mashamba ya serikali katika eneo la Ranchi ya Kalambo ( Kalambo Lanchi).

Maagizo hayo yametolewa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kupitia Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Alexander Mnyeti Machi 8,2025 wakati wa ziara yake Mkoani Rukwa iliyolenga kutembelea na kukagua mashamba ya serikali ya kulisha mifugo katika eneo la Ranchi ya Kalambo lenye vitaru 26.

Naibu waziri Mhe.Nyeti ameoneshwa kukerwa na tabia ya wananchi waliopewa maeneo na serikali kwa lengo la ufugaji na badala yake wameanzisha kilimo na kusema sio lengo la mashamba hayo huku akibainisha kuwa mashamba hayo ni kwaajili ya mifugo na hivyo kuwapa nafasi watu wenye nia ya kufanya shughuli za ufugaji.

“Walio omba vitaru hivi kwa ajili ya ufugaji waliowengi tumegundua wanafuna na kulima,wachache wanafuga lakini asilimia kubwa wanalima na wengine hawafugi kabisa na wengine tukiwapa mashamba,mashamba haya kwa kusingizia wanaenda kufuga lakini wamekwenda kukodishia wafugaji.

Mhe.Mnyeti amewataka wafugaji kuzingatia sheria, kanuni na utaratibu ili kuepusha migogoro kati ya wakulima na wafugaji “tunamashamba ya kulima malisho ya mifugo tungekuta malisho ya ng’ombe hapa tungeongeza na mitaji kwa sababu serikali inatoa ruzuku pia kwa wale ambao wanamashamba makubwa ili muweze kulima nyasi ng’ombe wetu wapate mazingira mazuri ya chakula,”alisema 

Akimwakilisha Mkuu wa Mkoa Mhe.Charles Makongoro Nyerere, Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Mhe.Nyakia Ally Chirukile amekemea kitendo cha wafugaji kuwazuia watumishi wa umma kutekeleza majukumu yao.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa wafugaj Tanzania Bw.Mrida Mshota Marucha amewataka wafugaji kulipa madeni wanayodaiwa ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za mifugo ikiwemo chakula cha mifugo.

Hata hivyo Bw.Marucha amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutoa kiasi cha fedha shilingi Bilioni 28 kwa ajili ya kuchanja mifugo.