Wakulima wa kijiji cha katumba Azimio kata ya Pito kijiji Manispaa ya Sumbawanga Mkoani Rukwa wamepatiwa elimu ya kilimo hai yenye lengo la kupambana na udumavu, pamoja na uhamsishaji wa utunzaji wa mazingira, vyanzo vya maji pamoja na namna bora ya kutengeneza na kutumia pembejeo za kilimo zizotumia kemikali.Elimu hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa shirika hilo Bw.Leonard Mwanjisi kupitia mafunzo yaliyowakutanisha wadau wa kilimo na wananchi mbalimbali wa kata ya pito kijiji cha katumba azimio katika ofisi ya lasilimali ya kilimo na mifugo Mkoani humo ambapo zaidi ya wakulima 60 wamenufaika na mafunzo hayo.
Katika mazungumzo yake Mwanjisi amesisitiza umhimu wa haki na usawa pamoja na ushirikishwaji wa familia katika nyanja za kiuchumi huku akiwataka kujiepusha na ulevi unaotajwa kushusha juhudi za uzalishaji.
Hata hivyo amewasihi wananchi hao kuzingatia utunzaji wa mazingira na vyanzo vya maji ili kuepusha athari zinazoweza kujitokeza ikiwa ni paomoja na ukame ambao husababisha njaa na magonjwa mengine.

Pia mwanjisi amelezea faida ya kilimo ikolojia ikiwa ni pamoja na kuvuna chakula kwa wingi kwa wakati mmoja hali itakayochagiza ukuaji wa uchumi katika familia na Taifa kwa ujumla huku akiwataka wakulima jinsia ya kiume kuacha ukatili wa kiuchumi kwenye familia zao na badala yake kujenga usawa katika mgawanyo wa lasilimali za kilimo.
Pamoja na hayo wananchi hao wameelekezwa namna ya kutengeneza na kutumia mbolea isoyokuwa na kemikali katika shughuli zao kilimo ambapo shughuli itasaidia kupunguza changamoto ya upatikanajii wa pembejeo za kilimo kwa wakulima wadogo wadogo.

Kwa upande wake Joseph Igogo Msemakweli Afisa kilimo amesema lengo la kilimo ikolojia ni kurudisha asili ya ardhi pamoja utunzaji wa vyanzo vya maji na viumbe hai.
Washiriki wa mafunzo hayo wameliomba shirika kuendelea kutoa elimu kwa wakulima wengini mkoani Rukwa ili kusaidia kuinua uchumi katika familia na taifa kwa ujumla “niombe kwa washiriki wengine tukawashirikishe na wengine maisha ni endelevu kwamba badala ya kula sumu tukale chakula kisicho kuwa na madhara,” alisema Nkyandawani.

Tunapatikana Kupitia