Watu sita wamefariki dunia na wengine 21 kujeruhiwa hapo jana 28 /6/2025 katika ajali iliyohusisha Toyota Hiace na bajaji katika mteremko wa Mlima Ulinji, uliopo Kijiji cha Ulinji, Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa.
Taarifa kwa umma iliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Makongoro Nyerere imesema Hiace ilipinduka katika Kata ya Mollo ambapo amesema waliofariki dunia ni watu wazima kiumri watatu (wanaume wawili na mwanamke mmoja) na watoto watatu (wavulana wawili na msichana mmoja).
Makongoro amesema miili imehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Rukwa. Kuhusu majeruhi amesema wanaume ni wanane na wanawake 13, ambao wamepelekwa katika hospitali hiyo kwa matibabu.
Katika hatua nyingine Mhe.Makongoro ametoa pole kwa ndugu jamaa na marafiki waliofikwa na msiba huo.
Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo, Dk Ismail Macha amethibitisha kupokea majeruhi na miili ya watu waliopoteza maisha huku akiwataka madereva wa vyombo vya moto kuwa makini wanapoedesha vyombo hivyo na wamiliki kuhakikisha vinakuwa salama wakati wote ili kuepuka ajali zinazoweza kuzuilika.
Bwana alitoa Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe Aminaaa.

Tunapatikana Kupitia