Na Fedrick Mbaruku - Rukwa

Kama ilivyo Shirika ni mkono wa pili wa serikali katika kufikia malengo kutokana na ushirikiano unaofanyika dhidi ya serikali na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali likiwemo shirika la ADEACH, zaidi ya Wakulima 80 wamepatiwa mafunzo ya kilimo ikolojia lengo likiwa ni kupambana na udumavu kwa kwa watoto wenze umri chini za miaka mitano.  

Mafunzo hayo yametolewa Julai 1 mwaka huu katika kata ya Kasense iliyopo Manispaa ya Sumbawanga Mkoani Rukwa kupitia Shirika la uwezeshaji Tanzania (SAT) kutoka Mkoani Morogoro kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo ya Kilimo na Afya ya Jamii (ADEACH) lililopo Mkoani Rukwa.

                             

Katika mafunzo hayo ya siku mbili yamewakutanisha wananchi na wadau mbalimbali wa kulimo ambapo pamoja na mambo mengine wamefundishwa namna ya utengenezaji wa mbolea, dawa ya kuua wadudu kwenye mimea isiyotumia kemikali ambapo ulaji wa vyakula vinavyo yalishwa kwa kutumia dawa na viuatilifu vingine kunatajwa kama sababu mojawapo ya udumavu.

Katika hatua nyingine wananchi hao wamepewa elimu juu ya kukabiliana na vitendo vya ukatili kwa watoto vinavyoendelea katika maeneo mbalimbali nchini kwa kuhakikisha wayayi na waleyi wanakuwa karibu na familia yao.

                                               

Mwezeshaji kutoka shirika la uweyeshaji Tanzania (SAT) Rashidi Raswiu amewapongeya wananchi hao kwa kushiriki mafunzo hayo na kuwataka kuzingatia waliyofundishwa na wataalam huku akisema kutokana na mwitikio wao SAT iataweka nguvu kwa wakulima wa Mkoa wa Rukwa ili kuwasaidia kufikia malengo yao.