Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mhe. Charlse Makongoro Nyerere ameipongeza Benki ya TCB (Tanzania Commercial Bank) kwa kufungua tawi jipya Sumbawanga mjini ilikuwasogezea huduma karibu wananchi wa mkoa wa Rukwa.

Mhe makongoro ametoa pongezi hizo katika hafla ya uzinduzi wa tawi jipya la benki ya TCB Sumbawanga mjini leo Julai 10,2025.

Mkuu huyo amesema Hatua hii ya kufungua tawi jipya hapa Sumbawanga inaonesha dhamira ya dhati ya benki hii katika kuwafikia wananchi popote walipo.



Aidha Mh makongoro amesema Nimefurahishwa pia na namna ambavyo mnaendelea kuongeza idadi ya mawakala– hatua inayowezesha wananchi hata wa maeneoya pembezoni kupatahuduma za kibenki kwa urahisi.

Kwa upande wa Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya TCB, Bw. Adam Mihayoamesem Kufunguliwa kwa tawi la Sumbawanga ni hatua muhimu katika kuhakikisha kila Mtanzania anapata huduma za kifedha bila ya vikwazo vya kijiografia.

Bw. Mihayo ameeleza pia kuwa TCB inaendelea kutoa mikopo nafuu kwa wakulima na wafanyabiashara wadogo na wa kati, ikigusa kila hatua ya mnyororo wa thamani wa kilimo na biashara.