Katika kuhakikisha jamii inapambana na udumavu nchini,Shirika la maendeleo ya kilimo na afya ya jamii (ADEACH) kwa kushirikiana na shirika la kilimo endelevu Tanzania (SAT) wameendelea kutoa mafunzo ya kilimo hifadhi kwa wakulima katika maeneo mbalimbali nchini.

Akizungumza na wananchi na wadau wa kilimo kwenye mafunzo yaliyofanyika katika shule ya Msingi Msua iliyopo Manispaa ya Sumbawanga Mkoani Rukwa Mkurugenzi wa shirika la Maendeleo ya Kilimo na Afya ya Jamii (ADEACH) Bw.Leonard Mwanjisi amesema Licha ya mkoa wa rukwa kutajwa kwenye orodha ya mikoa inayozalisha chakula kwa wingi lakini bado Mkoa huo unakabiliwa na tatizo la udumavu.

Mafunzo hayo yametolewa mkoani humo kwa nyakati tofauti ambapo jumla ya kata nne Mkoani humo zimefikiwa na mafunzo hayo ikiwemo kata ya Pito,Kasense,Milanzi na Kata ya Chanji ikiwa ni moja ya hatua madhubuti za kukabiliana na tatizo la udumavu kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano.



Kufuatia hatua hiyo la ADEACH kwa kushirikiana na Shirika la kilimo endelevu Tanzania SAT wameendelea kuunga mkono jitihada za kukabiliana na tatizo hilo la udumavu mkoani Rukwa kwa kutoa elimu ya kilimo hai kisichotumia kemikali ili kwa kuwafundisha wakulima namna ya kutengeneza mbolea na dawa ya kufukuza wadudu kwenye mimea.

Hatua inayo ilenga kuondoa ghalama katika uzalishaji sambamba na kuondokana na magonjwa mbalimbali ukiwemo ugonjwa wa kansa.

Amesema kilimo hai ni teknolojia ambayo inatumika kuzalisha mazao ambayo yanazalishwa kwa kutumia dawa zisizokuwa na kemikali huku akisema kilimo hicho kinasaidia pia katika uhifadhi wa mazingira,kilimo rafiki kwa mimea na kilimo rafiki kwa viumbe hai na hivzo kuwataka wananchi kutumia kilimo hicho ili kulinda lasilimali za asili.


Katika hatua nyingine Mwanjisi amesema kilimo hai ndio kilimo pekee ambacho kinasaidia kupambana na udumavu kwa watoto wenye umri wa miaka mitano,kupambana na magonjwa yanayotokana na ulaji wa vyakula vilivyoyalishwa kwa kutumia sumu kali.

Amesema mkoa wa rukwa unavyakula vingi lakini bado udumavu upo ambapo amewataka wananchi kuwa na utaratibu mzuri.

Wadau hao wamepatiwa mafunzo ya kutengeneza mbolea na dawa ya kufukuya wadudu mashambani zisizotumia kemikali.