Wito huo umetolewa na Afisa Tarafa ya Lwiche Bi. Dafroza Msechu, akimuwakilisha Katibu Tawala wa Wilaya ya Sumbawanga Bw. Gabriel Masinga, katika kongamano la vijana lililofanyika leo katika Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga. Kongamano lililowakutanisha vijana kutoka maeneo mbalimbali kwa lengo la kuelimishwa na kujadili fursa za maendeleo.
Bi. Dafroza amesema vijana ni tunu ya Taifa kutokana na nguvu walizopewa na Mwenyezi Mungu, akisisitiza kwamba iwapo watafanya kazi kwa bidii na ubunifu, maendeleo endelevu yataonekana kila siku.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga Frank J. Maten, ameeleza kuwa Halmashauri itaendelea kuandaa makongamano mbalimbali kwa ajili ya kuwaelimisha vijana kuhusu fursa mbalimbali zilizopo Nchini ili waweze kujihusisha katika shughuli za kiuchumi zenye tija.





Tunapatikana Kupitia