
Bonanza la Mpira wa Pete (Netball) lililofanyika leo Februari 28, 2026 katika Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga Mkoani Rukwa, limehitimishwa kwa mafanikio makubwa, likizikutanisha jumla ya timu saba kutoka maeneo mbalimbali ndani na nje ya Manispaa huku likiwa jukwaa muhimu la kukuza vipaji, kuimarisha ushirikiano na kuhamasisha ushiriki wa wanawake katika michezo.
Bonanza hilo limeweka thabiti ushindani mkubwa na wa kuvutia, ambapo timu zimeonesha nidhamu, uwezo na ushindani wa heshima ambapo matokeo yamekua kama ifuatavyo:
Luwa JKT 07 dhidi ya Matai Sekondari 26, Chuo cha Ualimu Sumbawanga 19 dhidi ya Shule ya Msingi Matai 06, Winner 25 dhidi ya Matai Sekondari 08, Songwe 27 dhidi ya Chuo cha Ualimu Sumbawanga 02, TANESCO 23 dhidi ya Luwa JKT 10, Winner 10 dhidi ya Songwe 21.
Bonanza hilo limeelezwa kuwa siyo tu sehemu ya mashindano ya michezo, bali pia ni jukwaa muhimu la kuonesha mshikamano, kukuza vipaji vya wanawake na kuimarisha afya pamoja na ustawi wa jamii kupitia michezo.



Tunapatikana Kupitia