Wafanyabiashara katika Soko Kuu la Kimataifa la Biashara Kariakoo, wamemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan, kwa kukamilisha ahadi ya ukarabati na ujenzi wa soko jipya.
Aidha, wamemkaribisha katika hafla ya uzinduzi wa soko hilo ambao utafanyika leo Februari 8,2026.
Serikali imetoa Sh. bilioni 28 za ukarabati na ujenzi wa soko jipya baada ya kuungua moto na kuteketeza mali za wafanyabiashara Julai 2021.
Soko hilo lina zaidi ya vizimba 1,500 vitakavyotumika na wafanyabiashara wadogo, wa kati na wakubwa, jambo litakaloongeza fursa za ajira na kuchochea ukuaji wa uchumi wa mkoa na Taifa kwa ujumla.
Tunapatikana Kupitia