Maafisa Usafirishaji wa Stendi ya Kiwira Wilaya ya Rungwe Mkoa wa Mbeya wamehimizwa umuhimu wa kuheshimu na kutii sheria za usalama barabarani bila shuruti ili kuepuka ajali
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Usalama barabarani Wilaya ya Rungwe Mrakibu wa Polisi (SP) Felix Kakolanya katika mkutano alioufanya Februari 7, 2026 Stendi ya Kiwira.
Aidha, SP Kakolanya amewataka Maafisa Usafirishaji hao kujiendeleza kielimu kwa kuhakikisha wanahudhuria mafunzo ya udereva ili kuwa mahiri na kuwajengea uwezo na uelewa wa sheria, alama na michoro ya usalama barabarani.
Mbali na hayo, SP Kakolanya amewataka Maafisa Usafirishaji kuzingatia sheria za upakiaji salama wa mizigo na kujiepusha na upakiaji wa mizigo kwenye Pikipiki kwa njia hatarishi kama vile Milango, Madirisha, Nondo, Mbao na vitu vingine kinyume na sheria.
Sambamba na hayo, amewataka kuheshimu watumiaji wengine wa barabara hasa kuheshimu vivuko vya watembea kwa miguu ili kuepuka ajali zinazoweza kuepukika kwa kutii na kufuata sheria.
.jpeg)

.jpeg)

Tunapatikana Kupitia