Polisi Kata wa kata ya Mlali Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro Mkaguzi wa Polisi Mwantumu Msilu amewaalika wadau mbalimbali kumsaidia mtoto Raphael Cristian aliyezaliwa na changamoto ya utumbo kutoka nje.
Mtoto Raphael anaishi na mama yake katika kitongoji cha Peapea MLali ambaye ametelekezwa na mumewe mara tu alipojifungua na kubainika kuwa mtoto anachangamoto hiyo, jambo ambalo lilimsukuma mama huyo kumtafuta Polisi kata na kuomba msaada.
Kwa upande wake mkaguzi Mwantumu amesema, mara baada ya kutafutwa na mama huyo alimsikiliza na kuingiwa na moyo wa huruma jambo lililomfanya amtafutie msaada kwa wadau mbalimbali.
Wadau waliojitokeza ni pamoja na Katibu wa Mbunge, Diwani wa Kata ya Mlali, pamoja na Wawakilishi wa kundi la wazalendo Morogoro na kukabidhi kiasi cha pesa cha kuanzisha matibabu lakini mtoto huyo bado anahitaji msaada zaidi na mama yake anapatikana kwa namba 0717749313.

.jpeg)


Tunapatikana Kupitia