Serikali imepunguza vifo vitokananvo na uzazi na uzazi kwa wajawazito kwa asilimia 80 kwa kipindi cha miaka saba kutoka vifo 556 kwa kila vizazi hai 100000 hadi vifo 104 kwa kila vizazi hai 100000


Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa mradi kutoka shirika la Thamini wakati wa utambulisho wa Mradi mama na mjamzito salama mkoani Geita.

Dkt. Sunday, amesema mradi huu wa miaka mitano utatekelezwa katika mikoa ya Kigoma, Katavi, na Geita. 

Dkt. Sunday ameongeza kuwa mradi huu unafadhiliwa na Bloomberg Philanthropies na Gates Foundation, wadau wa maendeleo wanaoshirikiana na Serikali katika sekta ya afya. 

Amesema wadau hao watashirikiana kwa karibu katika utekelezaji wa mradi ili kuchangia juhudi za serikali za kuhakikisha malengo ya kupunguza vifo vya mama na mtoto wakati wa kujifungua yanafikiwa, kuelekea utekelezaji wa Malengo Endelevu kufikia mwaka 2030