Mhe. Johari ameapa mbele ya Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Mahakama na Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. George M. Masaju, kufuatia kuteuliwa kuwa Mjumbe wa Tume hiyo.
Mwanasheria
Mkuu wa Serikali ameteuliwa kuwa mjumbe wa Tume ya Utumishi wa Mahakama
kufuatia kuteuliwa kwake kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa mara ya
pili na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu
Hassan Novemba, 2026.
Aidha, Mwanasheria Mkuu
wa Serikali ameapishwa kuwa Kamishna kutimiza takwa la Sheria ya
Usimamizi wa Mahakama Na. 4 Sura ya 237 inayomtaka kila Kamishna
kuapishwa na Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Mahakama kabla ya kuanza
kutekeleza majukumu yake.
Sambamba na Mhe.
Johari, Wajumbe wengine wa Tume ya Utumishi wa Mahakama walioapishwa ni
pamoja na Jaji wa Mahakama ya Rufaa Mhe. Gerson Mdemu, na Mawakili wa
Kujitegemea Bw. Thomas Nyanduga na Bi. Dorcas Mutabuzi.

Tunapatikana Kupitia