Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mh. Dr. Hussein Mwinyi amemtuku tuzo Polisi Kata wa Mbingu, Wilaya ya Kilombero Mkoani Morogoro Insp. Patrick Stanley kwa kutumia imani ya dini kuzuia uhalifu kupitia mashindano ya ya usomaji wa qur-an alioandaa kwenye kata yake.

Insp Patrick aliandaa  matukio mawili kwa mwaka 2024 na 2025 aliyoyapa jina la POLISI JAMII QUR -AN COMPETITION MBINGU ambapo ndani yake yalifanyika mashindano ya usomaji wa qur-an na POLISI JAMII CRISTIAN CONFERENCE MBINGU kwa upande wa Wakristo ambayo yalileta matokeo chanya kwa jamii ya Mbingu hasa eneo la uhalifu na maadili ikiwemo kukoma kwa ngoma za vigodoro zilizokuwa zikichangia mmomonyoko wa maadili kwa jamii na kupungua kwa uhalifu kutokana na ujumbe ulioambatana na tukio hilo

Kwa kutambua mchango huo tasisi ya AL HIKMA FOUNDATION THE GREATEST iliyoandaa mashindano ya kimataifa ya usomaji wa qur-an yaliyofanyika Machi 1,2026 ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Rais wa Mapinduzi ya Zanzibar Mh. Dr Hussein Mwinyi imemkabidhi tuzo kwa kutambua mchango wake huo mkubwa kwenye jamii.

Mashindano hayo yamefanyika katika uwanja wa Mkapa mkoani Dar es salaam na kuhudhuriwa na watu zaidi ya milion 60.