Kamishina mkuu wa mamlaka ya mapato tanzaniaTRA Bwa. Yusuph Juma Mwenda amewashukuru na kuwapongeza wafanza biashara wa mkoa wa Rukwa kwa ulipaji kodi wa hiari hali iliyo changia mkoa kuvuka lengo la kukusanya kodi kwa asilimia 130 kwa mwaka wa fedha ulioisha 2024/2025.

Mwenda amesema hayo katika kiko kilicho wakutanisha wafanya biashara wa mkoa wa Rukwa na kamishina mkuu huyo kilicho fanyika jana tarehe 3 Julai,2025 katika ukumbi mkubwa wa mikutano uliopo ofisi ya mkuu wa mkoa wa Rukwa.

Mbali na pongezi hizo Mwenda amewahakikishia wazabuni na wakandarasi wanaoidai serikali kuwa watalipwa madeni.

“Lazima madeni yenu ya ndani yalipwe na mimi nitakuwa balozi wenu hasa kwa wale wanaotudai kuwasema zaidi  wale wenye madeni na justification uwenda yapo wizara ya fedha,au yapo wizara mbalimbali kama ujenzi ili muendelee kulipa kodi sisi kama TRA tutakuwa mabalozi wenu kuwasemea,” kamishina mkuu TRA