Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araghchi amesema hakuna tarehe mpya iliyopangwa kwa sasa kwa ajili ya duru ijayo ya mazungumzo ya nyuklia na Marekani.

Aragchi ameitoa kauli hii alipokuwa akihojiwa na shirika la habari la Al Jazeera na ikiwa ni siku moja baada ya pande hizo mbili kufanya mazungumzo nchini Oman.

Mwanadiplomasia huyo mkuu wa Iran amesema mazungumzo ya Muscat yalikuwa  "chanya", huku Rais wa Marekani Donald Trump akiyasifu kuwa mazuri na pande zote mbili zimekubaliana kuendelea na mchakato huo.

Aidha, Araghchi amekosoa kile alichotaja kuwa "ubabe" wa Israel wa kuimarisha silaha zake za kijeshi huku ikizishinikiza nchi zingine katika eneo hilo kupokonywa silaha.