Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga, likiongozwa na Mwenyekiti wake ambaye ni Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo, Mhe. Frank Lupimo, limeketi kikaoni leo Februari 6, 2026 kwa lengo la kupitia na kujadili Mpango na Bajeti ya Manispaa kwa mwaka wa fedha 2026/2027.

Katika kikao hicho, Baraza limepitisha rasimu ya bajeti yenye jumla ya makisio ya Tshs. 51,078,890,654 kwa mwaka wa fedha 2026/2027, ikiwa ni ongezeko la Tshs. 219,559,654 ikilinganishwa na bajeti ya mwaka 2025/2026 ambayo ilikuwa na makisio ya Tshs. 50,859,331,000.

Hatua ambayo ni muhimu katika kuelekea utekelezaji wa mipango ya maendeleo endelevu kwa wananchi wa Manispaa ya Sumbawanga.