Mkuu wa
Wilaya ya Ileje, Farida Mgomi, ametoa rai kwa wananchi kujenga utamaduni wa
kujitolea damu kwa hiari ili kuokoa maisha ya wajawazito na watoto wachanga wanaohitaji
huduma za dharura.
DC Mgomi ametoa kauli hiyo wakati akifungua kikao kazi cha siku mbili cha
mapitio ya vifo vitokanavyo na uzazi na vifo vya watoto wachanga kwa Mkoa wa
Songwe kilichowakutanisha wataalamu wa afya kutoka wilaya zote za mkoa huo.
Amesema upatikanaji wa damu salama na ya kutosha ni moja ya nyenzo muhimu
katika kupunguza vifo vinavyoweza kuzuilika, na akasisitiza kuwa utoaji damu ni
tendo la upendo na uzalendo linalopaswa kupewa kipaumbele kama ilivyo sadaka
katika nyumba za ibada.
Aidha, amewataka wataalamu wa afya kuendelea kutoa elimu kwa jamii kuhusu
umuhimu wa uchangiaji damu wa hiari ili kuhakikisha vituo vya afya vinakuwa na
akiba ya kutosha muda wote kwa ajili ya dharura.


Tunapatikana Kupitia