"Hatuendi kwenye mechi ngumu, tunaenda kwenye mechi muhimu. Mechi ngumu tulishamaliza dhidi ya Al Ahly, hawa FAR RABAT tunawamudu, hatutakiwi kuwa na chembe ya hofu wala wasi wasi wowote, tunatakiwa kwenda pale kwa mentality ya kupata matokeo"
"Tumeondoka wote, hatujaacha mtu ofisini, kuna walioondoka jana, leo na wengine wanaondoka kesho, tunaenda wote ili pasitokee mahali pakapwaya.
Nyie mnaweza msiamini ila mentality ya Yanga ni kwenda kushinda pale pale, akili yetu inatutuma hivyo na uwezo tunao"
Ally Kamwe , Meneja Habari Na Mawasiliano wa Klabu ya Yanga akizungumza wakati klabu ya Yanga ikiondoka kuelekea Morocco kwa mchezo dhidi ya ASFar Rabat.

Tunapatikana Kupitia