Macron amesema katika mahojiano na magazeti kadhaa ya Ulaya yaliyochapishwa hii leo kwamba Ulaya haipaswi kuwaachia Urusi na Washington mazungumzo hayo.
Msemaji wa Ikulu ya Kremlin Dmitry Peskov amethibitisha kuwepo kwa mawasiliano na kusema Urusi iko tayari kurejea kwenye mazungumzo na Ufaransa, katika ngazi ya rais.
"Tunaweza kuthibitisha kwamba kumekuwepo na mawasiliano, ambayo ikiwa yatahitajika na ni lazima yanaweza kusaidia kuanzisha mara moja mazungumzo ya ngazi za juu. Hadi sasa, hatujaona nia yoyote, ingawa tumeona kauli ya Macron kuhusu hitaji la kuanzisha uhusiano na Urusi."
Rais Vladimir Putin mara kadhaa ameitetea Urusi kwamba haikuvunja uhusiano, bali ni mataifa ya Ulaya.

Tunapatikana Kupitia