Msemaji wa shirika hilo Ravina Shamdasani amewaambia waandishi wa habari mjini Geneva kwamba, mkuu wa shirika hilo Volker Turk aligusia hilo alipozungumza na rais wa mpito wa Venezuela Delcy Rodriguez Januari 26.
Amesema kwenye mazungumzo yao Turk alimuahidi rais huyo wa mpito kuisaidia Venezuela kuandaa mpango wa mazungumzo na maridhiano, ambapo suala la haki za binadamu litatiliwa kipaumbele.
Akaongeza pia ana nia ya kufungua upya ofisi za shirika hilo na tayari alituma timu iliyozuru Caracas hadi Februari 4, ambayo ilikutana na makundi mbalimbali ikiwa ni pamoja na watetezi wa haki za binaadamu.

Tunapatikana Kupitia