Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Kamishna Msaidizi Mwandanizi wa Polisi (SACP) Augustino Senga, amewapongeza askari tisa (09) wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia Mkoa wa Songwe kwa kuhitimu fani mbalimbali za taaluma za Polisi. Askari hao walihitimu katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam tarehe 29 Januari, 2025, katika mahafali ya kumi (10) kwa mwaka wa masomo 2024/2025.
Pongezi hizo zilitolewa tarehe 03 Februari, 2026 katika Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, ambapo Kamanda Senga aliwasisitiza wahitimu hao kutumia elimu na ujuzi walioupata katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku, huku akiwasisitiza umuhimu wa kutoa huduma bora kwa wananchi ili kuendelea kujenga na kudumisha taswira chanya ya Jeshi la Polisi.
.jpeg)
Aidha, Kamanda Senga aliwataka askari hao kuhakikisha wanaitendea haki elimu waliyoipata kwa kutekeleza majukumu yao kwa weledi, uadilifu na kujali maslahi ya wananchi, kama ilivyokusudiwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania.
Vilevile, Kamanda Senga aliwahimiza askari hao, kuwa mstari wa mbele katika utekelezaji wa majukumu yao, kuwa vinara wa nidhamu na utendaji bora, na kuwa mfano na kioo kwa askari wengine ili wawe kama wao, ikiwa hatua hiyo itaendelea kuimarisha huduma bora na imani ya Jeshi la Polisi na jamii kwa ujumla

.jpeg)

.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)
Tunapatikana Kupitia