Dirisha la usajili wa Januari 2026 limefungwa rasmi nchini England na katika ligi nyingine kubwa duniani, likiacha nyuma yake mchanganyiko wa dili za kushangaza, maamuzi ya kimkakati na uhamisho uliotikisa mashabiki.

Tofauti na Januari nyingi zilizopita ambazo mara nyingi huonekana tetesi nyingi, safari hii vilabu kadhaa hasa vya Ligi Kuu ya England vilichukua hatua kubwa kifedha, vikihusika katika uhamisho wa wachezaji waliogharimu mamilioni ya pauni.

Kwa mujibu wa takwimu za soko la usajili, vilabu vya ligi kuu England vilihusika katika uhamisho saba kati ya kumi ghali zaidi duniani kwa mwezi Januari, ishara nyingine ya nguvu yao ya kifedha katika soka la kisasa.

Hawa hapa ni wachezaji 10 waliotikisa zaidi dirisha la usajili wa Januari 2026, si kwa thamani pekee, bali pia kwa uwezo wao ndani na nje ya uwanja