.jpeg)
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Mheshimiwa Charles Makongoro Nyerere, ametoa wito kwa wawekezaji wa ndani, wafanyabiashara, wajasiriamali, vijana kutumia kikamilifu fursa za uwekezaji zilizopo mkoani humo ili kuchochea ukuaji wa uchumi wa mtu mmoja mmoja na Mkoa kwa ujumla.
Ametoa wito huo leo Februari 24,2026 wakati akifungua rasmi semina ya uwekezaji iliyoandaliwa na Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA), amesema kuwa lengo la Semina hiyo ya kitaifa ni kuhamasisha uwekezaji wa ndani na kubadili mtazamo wa watanzania kwamba uwekezaji ni wa wageni pekee.
Mheshimiwa Makongoro Nyerere amesema kuwa Mkoa wa Rukwa ni hazina ya fursa za uwekezaji ambazo bado hazijatumika kikamilifu. Katika kilimo, mazao ya kimkakati kama parachichi, alizeti, soya, kahawa, mpunga na mahindi yana soko la uhakika ndani na nje ya nchi, yakitoa msingi imara wa uwekezaji katika uzalishaji wa kisasa na hasa viwanda vya uchakataji ili kuongeza thamani na mapato ya wakulima.

Aidha, sekta ya mifugo na uvuvi ina nafasi pana kupitia ranchi zinazofaa kwa ufugaji wa kisasa na unenepeshaji kwa soko la kimataifa, pamoja na ufugaji wa samaki kwa mfumo wa vizimba na matumizi ya zana bora za uvuvi kwa ajili ya uendelevu. Utalii unahitaji hoteli za kisasa na nyumba za kulala wageni ili kuhudumia wageni wanaovutiwa na vivutio vya asili, wakati sekta ya madini ikitoa fursa kupitia rasilimali kama emerald, makaa ya mawe, dhahabu, shaba na gesi ya helium.
Kwa mtazamo wa kimkakati, Rukwa ni lango la uwekezaji lenye uwezo wa kuleta mageuzi ya kiuchumi kwa kasi.
.jpeg)
Mheshimiwa Makongoro, Nyerere amesema uwekezaji wa ndani una maana kwa kuongeza ajira kwa vijana, kipato kwa familia na kupanuka kwa wigo wa kodi zinazorejeshwa katika huduma za kijamii.
Amebainisha kuwa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa itaendelea kuweka mazingira wezeshi, ikiwemo kutenga maeneo mahsusi ya uwekezaji wa viwanda katika wilaya zote na kushughulikia changamoto zinazowakabili wawekezaji.

.jpeg)


.jpeg)

.jpeg)
Tunapatikana Kupitia