Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kimesema hakipendezwi na tabia ya baadhi ya mawakili kupokea malipo kutoka kwa wateja bila uwajibikaji unaofaa, na kuhimiza kuwa wote wanaofanya kazi za uwakili wahakikishe wanazingatia kwamba taaluma yao ni Ibada yenye uwajibikaji mkubwa kwa jamii.
Akizungumza leo 2 Februari 2026, jijini Dodoma, wakati wa maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini, Rais wa TLS, Wakili Boniface Mwabukusi ameweka bayana kuwa Shule ya Sheria (Law School) inapaswa kuchunguzwa kwa ukaribu kupitia michakato yake ya kuandaa mawakili, ili kuhakikisha kwamba vinara wa taaluma hiyo ni mawakili waadilifu na wenye sifa stahiki.
“Kwa sababu sio lazima kila mtu awe wakili,kama hawezi akafanye tu kazi nyingine na tuweke utaratibu wa kujua kuwa uwakili ni ibada,sio sheria tu tunawajibika kwa Mungu’Alisema Mwabukusi
Aidha, Mwabukusi ameiomba serikali iimarishe shule hiyo kwa kuweka vikwazo vya kina ili kuzuia watu wasiofaa kuingia kwenye taaluma ya uwakili.

Tunapatikana Kupitia