Waziri wa Afya, Mohamed Mchengerwa, leo Februari 2, 2026, amezindua rasmi mashine ya uchunguzi ya kisasa ya PET-CT Scan pamoja na huduma ya miadi mtandaoni katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI), Dar es Salaam. Uzinduzi huo ni sehemu ya jitihada za serikali za kuimarisha mifumo ya afya kupitia teknolojia na uwekezaji katika vifaa vya kisasa, ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma za afya za viwango vya kimataifa ndani ya nchi.
Mashine hiyo ni ya kwanza nchini, na awali wananchi walilazimika kusafiri nje ya nchi kupata vipimo vya aina hiyo.
Mashine ya PET-CT Scan, yenye thamani ya shilingi bilioni 18.7, ina uwezo wa kugundua mapema saratani na kufuatilia ugonjwa, huku ikitumikia wagonjwa zaidi ya 500 kila mwaka.
Huduma hiyo pia itapunguza gharama kubwa zinazotumika kwa wagonjwa kusafiri kwenda India, ambapo wastani wa kipimo ni shilingi milioni 1.2.
Waziri Mchengerwa amewaalika Watanzania wote kutumia huduma hiyo katika Taasisi ya Saratani ya Ocean ili kufanyiwa uchunguzi wa kisasa.
Tunapatikana Kupitia