Wadau wa
Elimu katika Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga leo Februari 10, 2026
wameketi kikaoni kujadili masuala mbalimbali ya elimu katika shule za
Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga kwa lengo la kuimarisha mazingira
ya ufundishaji na ujifunzaji.
Kikao kilichowaleta pamoja Wataalam
wa Mkoa, Halmashauri, Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya
Sumbawanga, Watendaji wa Kata, Maafisa Elimu, Wakuu wa Shule, Walimu
Wakuu pamoja na Wazee Mashuhuri wa Mkoa wa Rukwa. Kupitia kikao
hicho kilichoongozwa na Mwenyekiti wake, Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga
Mhe. Nyakia Ally Chirukile amesisitiza uzalendo wa ufundishaji kwa
Walimu wa shule za Sekondari na Msingi ili kuinua ufaulu kwa Wanafunzi
na kudumisha matokeo chanya yanayopatikana katika Manispaa ya
Sumbawanga.
Katika kikao hicho, Mhe. Chirukile ameipongeza
Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga kwa kuongoza Mkoa wa Rukwa katika
ufaulu wa Mtihani wa Kidato cha Nne 2025 na Mkoa wa Rukwa kuwa nafasi ya
Tisa Kitaifa katika Mtihani wa Kidato cha Nne 2025, akieleza kuwa
mafanikio hayo ni matokeo ya mshikamano wa Serikali, wadau wa elimu,
juhudi za Walimu pamoja na usimamizi thabiti wa Sekta ya Elimu ndani ya
Manispaa na kusisitiza kuwa elimu ipewe kipaumbele kuanzia sasa.
Mhe.
Chirukile ameongeza kuwa ushirikiano baina ya Serikali, Viongozi wa
Siasa pamoja na Wazee mashuhuri na wa Mila ni muhimu katika kuongeza
msukumo juu ya uelewa wa Jamii kuzingatia elimu kwa kupeleka watoto
shule na kusimamia maendeleo ya Wanafunzi.
Pamoja na hayo Mhe.
Chirukile amesema kuwa Watoto wakipelekwa shule itaondoa wimbi la Watoto
Mitaani ambao watapata ujuzi utakaosaidia maarifa kwa maendeleo
endelevu.
Katika hatua nyingine, Mhe. Chirukile amesema kuwa
Serikali inaendelea kuwekeza miundombinu bora ya elimu, vifaa vya
kufundishia, Walimu pamoja na lishe shuleni, hali ambayo kwa sasa
imeendelea kuimarika kila siku na kuchangia matokeo chanya katika Sekta
ya Elimu.
Tunapatikana Kupitia