Ofisi za Ufaransa za X ya Elon Musk zimevamiwa na kitengo cha mwendesha mashitaka wa Paris wa uhalifu wa mtandaoni, ikiwa ni sehemu ya uchunguzi wa makosa yanayoshukiwa ikiwa ni pamoja na uchimbaji wa data kinyume cha sheria na kushiriki katika kupatikana na ponografia ya watoto.

Ofisi ya mwendesha mashtaka ilisema uchunguzi ulianza Januari 2025 ulipoanza kuchunguza maudhui yaliyopendekezwa na mfumo wa mtandao wa kijamii, kabla ya kupanuliwa ili kujumuisha gumzo lake la utata la AI, Grok.

Katika taarifa yake, iliongeza kuwa Musk na mtendaji mkuu wa zamani wa X Linda Yaccarino wameitwa kuhudhuria vikao vya kesi mwezi Aprili.

X bado hajatoa maoni yake lakini hapo awali ametaja uchunguzi huo kama shambulio dhidi ya uhuru wa kujieleza.