Wananchi wa Kijiji cha Katete kata Myunga Wilaya ya Momba Mkoa wa Songwe wamekumbushwa umuhimu wa kushirikiana na viongozi wa kata katika kuhakikisha maeneo yote ya kata yanakuwa salama.

Akizungumza tarehe 10 Februari 2026, na wananchi hao Polisi Kata wa Myunga Mkaguzi wa Polisi Kiende Mshana, aliwahimiza wananchi hao kutoa taarifa mapema wanapoona viashiria vya uhalifu na kushiriki kikamilifu katika shughuli za ulinzi shirikishi kwa kushirikiana na viongozi wa Vijiji na kata ili Kijiji cha Katete kiendelee kuwa salama.
 
Kwa niaba ya wananchi hao, Severine Slaa aliahidi kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kudumisha amani, kushirikiana na viongozi wao pamoja na kuhakikisha kijiji na kata kwa ujumla vinaendelea kuwa salama na tulivu kwa maendeleo ya jamii.