Wajichimbaji wadogo wadogo wadini wa  kata ya Mbangala Wilaya na Mkoa wa Songwe wamekumbushwa umuhimu wa kuvaa vifaa kinga wakati wakiwa kwenye shughuli zao uchimbaji madini ikiwa ni pamoja na madhara ya matumizi ya dawa za kulevya kwani ni chanzo kikubwa cha matukio ya uhalifu katika kazi zao za kila siku. 

Wito huo umetolewa tarehe 10 Februari, 2026 na Polisi Kata ya Mbangala Mkaguzi wa Polisi Peter Selemani , aliwataka wajimbaji hao kuachana kabisa na matumizi ya dawa za kulevya na kuzingatia matumizi ya vifaa kinga wakati wa kuchimba madini hasa katika kipindi cha mvua nyingi ili kuepuka ajali na madhara mbalimbali yanayoweza kuepukika.

Pamoja na mambo mengine, Mkaguzi Selemani  aliwahimiza wachimbaji hao kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa za viashiria vya uhalifu na wahalifu ili kujenga jamii salama na yenye uchumi na ustawi endelevu.