Baraza la madiwani Wilayani Nkasi Mkoani Rukwa, limewachukulia hatua za kinidhamu watumishi wawili wa kada ya Afya kwa kuwafukuza kazi kwasababu ya utoro wa muda mrefu katika vituo vyao vya kazi
Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa kikao cha Mashauri ya kinidhamu kilichoketiwa na madiwani hao, Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mhe.Richard Leonard Masai alisema wamejiridhisha na taarifa za watumishi hao za kuwa watoro wa muda mrefu katika maeneo yao yakazi, hivyo wanakila sababu ya kuwafukuza kazi ili iwe fundisho kwa wengine.
Watumishi waliofukuzwa kazi ni Lyangawe Charles Lutu muuguzi daraja la II kituo cha afya Kirando na Gaudensia Fredrick Lukago muuguzi msaidizi daraja II kituo cha afya Kabwe

Tunapatikana Kupitia