Baraza la madiwani la Halmashauri ya wilaya ya Nkasi Mkoani Rukwa,  leo February 11, 2026, limepitisha mapendekezo ya rasimu ya mpango na bajeti ya Halmashauri hiyo kwa Mwaka wa fedha 2026/2027 ambapo Halmashauri inakadiria kukusanyana na kutumia jumla ya shilingi billion 47.3.

Akiwasilisha mapendekezo ya rasimu ya mpango na bajeti Afisa Mipango wa Halmashauri hiyo Ndg. Steward Vidoga, alisema mapendekezo ya bajeti yamelenga kutekeleza shughuli mbalimbali za Kutoa huduma za jamii, kuboresha miundombinu na kuongeza ukusanyaji wa mapato ya ndani kwa asilimia 100 ya makisio ya mwaka 2026/2027.

Aidha kupitia baraza hilo waheshimiwa madiwani,  wamejadili mapitio ya mpango na bajeti kwa kipindi cha nusu mwaka wa fedha 2025/2026, kuanzia July hadi Disemba, ambapo wamempongeza Mkurugenzi Mtendaji Ndg. Afraha N. Hassan kwakusimamia mapato na shughuli mbalimbali za maendeleo kwakipindi ambacho hakukuwa na Baraza la madiwani.