Watumiaji wa vyombo vya moto Mkwajuni wapewa elimu kuhusu masuala ya usalama barabarani elimu hiyo ilitolewa kwa  madereva na abiria vyombo vya moto wote walikumbushwa umuhimu wa kuzingatia sheria na tahadhari ili kulinda maisha ya abiria na mali, hususani katika barabara za vumbi zinazotumika katika eneo hilo la Mkwajuni wilaya na mkoa wa Songwe.

Akizungumza Machi 29, 2026, Mkaguzi wa Polisi Stella Rwekwama alitoa elimu kuhusu umuhimu wa kuendesha vyombo vya moto kwa mwendo mdogo hasa katika barabara za vumbi na wakati chombo kimebeba mzigo mzito. Alieleza kuwa mwendo kasi katika mazingira hayo unaweza kusababisha chombo kupinduka na kuhatarisha maisha ya abiria pamoja na mali.

Alihitimisha kwa kuwataka madereva kuzingatia usalama wa abiria kwa kuhakikisha hawakai kwenye guta au kuchanganywa na mizigo, kwani kufanya hivyo ni hatari na kunaweza kusababisha ajali. Pia aliwahimiza kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kupunguza ajali na kulinda maisha ya wananchi.