Wafanyabiashara pamoja na wateja wa nyama wajengewa uelewa na Polisi Kata wa Ilolo iliyopo Wilayani ya Mbozi mkoa wa Songwe, ambapo alietembelea bucha la nyama lililopo maeneo ya Ikonongo Mwizya na kuzungumza na wafanyabiashara pamoja na wateja kuhusu masuala ya usalama na afya ya jamii.
Alitoa wito huo Machi 29, 2026 katika bucha hilo, Mkaguzi wa Polisi Aggrey Mbogo alitoa mada kuhusu kupiga vita wizi wa mifugo na kuwataka wafanyabiashara kutonunua ng’ombe wa wizi. Alisema kuwa ushirikiano wa wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla ni muhimu katika kusaidia vyombo vya usalama kudhibiti vitendo vya wizi wa mifugo vinavyoweza kuathiri wafugaji na uchumi wa jamii.
Aidha, aliwataka wafanyabiashara kuzingatia usalama na afya ya jamii kwa kuhakikisha nyama ya ng’ombe inapimwa na wataalamu husika kabla ya kuuzwa kwa wananchi ili kuthibitisha kuwa inafaa kwa matumizi ya binadamu, pamoja na kuendelea kushirikiana na vyombo vya usalama kutoa taarifa kuhusu vitendo vya uhalifu vinavyojitokeza katika maeneo yao.



Tunapatikana Kupitia