Mahakama ya Wilaya ya Tunduru imemuhukumu James Hashimu Chingwaru,  (20) Mkazi wa Kijiji Cha Mtina - Tunduru kwenda Jela miaka 30 chini ya K/F 132 (1),(2) (a) Sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 R.E 20222 baada ya kukutwa na hatia kwa kutenda  kosa la kujaribu kumbaka bibi wa miaka 75.

Hukumu hiyo imesomwa Machi 16,2026 na Hakimu  Mhe, F.M Philip- PRM wa Mahakama ya Wilaya Tunduru baada ya mtuhumiwa kutenda kosa  hilo Desemba14,2025 huko kitongoji Cha Nyerere, Kijiji cha Mtina Wilaya ya Tunduru na kufikishwa mahakamani  Januari,13.2026 kwa hatua za kisheria.