✅Hali ya usalama katika daraja linalounganisha Kijiji cha Madibila, Kata ya Mambwe Kenya, Wilayani Kalambo ni ya kutisha na haivumiliki. Hiki ndicho kivuko kikuu cha Mto Momba (Saise), kinachounganisha vitongoji vya Mchese na Isale.
KWA NINI TUNAPIGA KELELE
🎓 Hatari kwa Wanafunzi: Kila kukicha, watoto wadogo wanalazimika kucheza kamari na maisha yao wakivuka daraja hili kufuata elimu. Je, tunasubiri mtoto apotee ndipo tuchukue hatua?
🏥 Kikwazo cha Huduma za Afya: Wananchi, wakiwemo wagonjwa na akina mama wajawazito, wanategemea kivuko hiki kufika vituo vya afya. Katika hali ya dharura, hapa ndipo maisha yanapopotelea.
🚜 Uchumi Unadumaa: Maendeleo ya kijiji yanategemea muingiliano wa watu na bidhaa. Miundombinu hii mibovu ni adui wa uchumi wa mwananchi wa kawaida.
Ujumbe kwa Viongozi Wetu:
Mh. Diwani Kelebi Sichilya, wananchi wako wanateseka na wanaishi kwa hofu kubwa. Hili daraja lipo ndani ya kijiji chako unachotoka, ni fedheha kuona hali hii ikiendelea huku kukiwa na uwezekano wa kurekebisha.
"Je, mpaka damu imwagike ndipo ukarabati ufanyike?"
Tunatoa mwito kwa Uongozi wa Mkoa wa Rukwa, TARURA, na wadau wa maendeleo kutazama hili kwa jicho la kipekee. Usalama wa mwananchi ni kipaumbele namba moja na ni haki ya msingi.
Tafadhalini naamini humu ndani kuna Viongozi wa vyama mbalimbali Tusaidieni kuokoa Maisha ya Wapendwa wetu


Tunapatikana Kupitia