Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mheshimiwa Patrobas Katambi amesema serikali uokoa kiasi cha Shilingi Bilioni 21 kwa ajili ya kulisha wafungwa kwa Utekelezaji wa Sheria ya Vifungo vya Nje ambayo imekuja kupunguza idadi ya wafungwa walioko magerezani.
Amesema jumla ya wafungwa 5000 wako katika Vifungo vya Nje huku wakitekeleza adhabu mbalimbali ikiwemo ushiriki wao katika kazi za kijamii katika ofisi za umma kote nchini.
Ametoa kauli hiyo baada ya kumaliza Kikao kazi na Kamati ya Taifa ya Huduma kwa Jamii inayoongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo na Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Morogoro,Mheshimiwa Jaji Stephen Magoiga.
Kikao hicho pia kilihudhuriwa pia na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Uangalizi,Asha Katembo na Mjumbe wa Kamati ya Taifa ya Huduma kwa Jamii,Aloyce Musika.
Kikao hicho kimefanyika Ofisi ndogo ya waziri,jijini Dar es Salaam.

Tunapatikana Kupitia