
Wafanyabiashara wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga wametakiwa kuwa mstari wa mbele kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo ya jamii, ikiwa ni jitihada za kuongeza kasi ya maendeleo endelevu kwa wananchi.
Wito huo umetolewa leo Machi 25, 2026 na Katibu Tawala wa Wilaya ya Sumbawanga, Bw. Gabriel Masinga, wakati akiongoza kikao na wafanyabiashara wanaojishughulisha na usafirishaji wa mizigo, ambapo amemuwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga, Mhe. Nyakia Ally Chirukile.
Akizungumza katika kikao hicho Bw. Masinga amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya Serikali na sekta binafsi, akibainisha kuwa wafanyabiashara wana nafasi kubwa katika kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika eneo hilo.
Kwa upande wao, wafanyabiashara wanaojishughulisha na usafirishaji wa mizigo wameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwezesha mazingira bora ya biashara sambamba na ujenzi wa miundombinu ya barabara hali inayosaidia kufanya kazi yao kwa weledi.



Tunapatikana Kupitia