
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, leo Machi 8, 2026 ametembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Soko la Kimataifa la Mazao Kanondo lililopo Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga Mkoani Rukwa.
Ujenzi wa soko hili unatekelezwa kupitia Mradi wa TACTIC kwa gharama ya Shilingi Bilioni 7.3, na hadi sasa umefikia asilimia 82 ya utekelezaji.
Soko hili linatarajiwa kuwa kitovu muhimu cha biashara ya mazao, likiwaunganisha wakulima, wanunuzi wakubwa, wasafirishaji na wawekezaji, hatua itakayopanua mtandao wa biashara na kuongeza thamani ya mazao ya wakulima wa Rukwa na maeneo jirani.



Tunapatikana Kupitia