Vyombo vya habari vya Kanisa Katoliki vimetakiwa kusimamia ukweli na kuepuka kujiingiza katika mtego wa kusambaza habari za uongo au zinazopotosha ukweli kwa maslahi binafsi na kutafuta umarufu wa kupata wasikilizaji na wasomaji au fedha.
Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Kurugenzi ya Mawasiliano ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Mhashamu Eusebius Nzigilwa, Askofu wa Jimbo Katoliki Mpanda na Makamu wa Rais TEC, wakati akifungua mkutano wa wadau wa vyombo vya habari vya Kanisa.
“Msiuze Kanisa kwa kutafuta umaarufu au fedha. Ukweli ubaki kuwa ukweli hata kama watu wote wataukataa, Habari za uongo zinasambaa kwa kasi kubwa, lakini vyombo vya habari vya Kanisa visiingie kwenye mtego huo.” alisema.
Askofu Nzigilwa alisema changamoto ya habari za uongo imeendelea kukua katika jamii huku baadhi ya watu wakigeuza ukweli na kuusambaza kwa makusudi, akifananisha hali hiyo na tukio la ufufuko wa Yesu Kristo ambapo walinzi walishawishiwa kuficha ukweli kwa kusema mwili wa Yesu uliibwa badala ya kukiri kuwa alifufuka.
Amesisitiza kuwa jukumu kuu la vyombo vya habari vya Kanisa ni uinjilishaji, huku akibainisha kuwa vifaa vya kisasa pekee haviwezi kufanya kazi hiyo kwa ufanisi bila mhusika kuwa na ukaribu wa kweli na Kristo.
“Uhusiano wako na Kristo ndiyo nyenzo kubwa ya utendaji wako wa kila siku. Maisha yetu na uthabiti wa imani yetu ndivyo vitakavyowavuta watu kwa Kristo kuliko maneno pekee,”
Chemchemi Sumbawanga
92.2fm

Tunapatikana Kupitia