Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi imeendelea na zoezi la ugawaji wa nyavu za kisasa kwa wavuvi wadogo wadogo kama sehemu ya juhudi za kukuza uchumi wa bahari na kuendeleza maisha ya jamii za wavuvi.
Zoezi hilo lilmefanyika katika kijiji cha kipili kata ya kupili wilayani nkasi Mkoani Rukwa , ambapo balozi wa kupinga uvuvi haramu Bwn.Paschal Mwakatenya alikabidhi nyavu pisi sita ambazo zitatumiaka kwa muda wa siku sita hadi saba kwa majaribio.
Amesema kuwa katika majiribio hayo anaamini kuwa nyavu hizo zitaleta faida kubwa na zitazuia uvuaji haramu kwani zimetengenezwa kwa ubora na viwango vya kitaifa.

“Nyavu hizi ni rafiki kwa mazingira na zitawasaidia wavuvi kuvua kwa tija bila kuathiri mazalia ya samaki. Serikali inatambua mchango wa wavuvi wadogo katika uchumi, ndiyo maana tunashirikiana nao kwa karibu zaidi,” .
Wavuvi waliopokea nyavu hizo wameishukuru serikali kwa msaada huo, wakieleza kuwa vifaa hivyo vitawasaidia kuongeza kipato na kuboresha maisha ya familia zao.
Mpango wa ugawaji wa nyavu umefanyika kwa mikoa ya Rukwa Kigoma na Katavi huku ukilenga zaidi wanawake na vijana wanaojishughulisha na uvuvi.
Uvuvi haramu umegeuka kuwa janga kubwa la kiuchumi na kimazingira ambapo kila mwaka mataifa ya afrika mashariki yanapoteza zaidi ya dola za marekani millioni 415 kutokana na uhalifu wa majini ambapo tanzania pekee inafikia hasara ya dola miliion 142.8.

Tunapatikana Kupitia