Wananchi wa Kata ya Kipili, Wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa, wameishukuru Serikali baada ya kukabidhiwa boti mpya ya Jeshi la Polisi yenye thamani ya shilingi milioni 300 kwa ajili ya kuimarisha ulinzi katika ukanda wa Ziwa Tanganyika.
Makabidhiano ya boti hiyo yalifanyika Agosti 28, 2025 katika kikosi cha Wanamaji Kipili, yakiongozwa na Mkuu wa Kikosi cha Wanamaji Polisi nchini, SACP Moshi Sokoni, aliyemkabidhi Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, SACP Shadrack Masija, mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Nkasi, Mhe. Peter Lijualikali.
Boti hiyo ni miongoni mwa boti 11 zenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 4.5 zilizotolewa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa Jeshi la Polisi, kwa lengo la kudhibiti uhalifu wa majini.
Kamanda Masija amesema boti hiyo itatumika na vyombo vyote vya ulinzi na usalama kwa ushirikiano, huku akiwasisitiza askari kuilinda na kuisimamia ipasavyo ili iwe na manufaa kwa wananchi.








Tunapatikana Kupitia