Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Rukwa kimezindua rasmi kampeni zake za uchaguzi, ambapo mgeni rasmi, Mwenyekiti wa chama hicho mkoani humo, Ashlafu Maufi, amewaomba wananchi kuendelea kukipa ridhaa chama hicho ili kiendelee kushika dola.
Akihutubia mamia ya wananchi waliohudhuria mkutano huo, Maufi amesema CCM imeendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika sekta za elimu, afya, maji, barabara na kilimo, jambo linalothibitisha dhamira ya chama hicho katika kuinua maisha ya wananchi.
Aidha, viongozi wa dini waliopata nafasi ya kuzungumza katika mkutano huo wametoa wito kwa wanasiasa wote kufanya siasa za kistaarabu zisizogawa wananchi kwa misingi ya dini, kabila au itikadi, ili kudumisha amani na mshikamano wa taifa.
Uzinduzi huo wa kampeni ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa CCM na jumuiya zake, pamoja na wananchi kutoka maeneo tofauti ya mkoa wa Rukwa.



Tunapatikana Kupitia