:Mgombea mwenza wa kiti cha  urais kupitia chama cha mapinduzi CCM amesema chama kimejikita katika kugusa sekta ambazo zinakwenda kuikuza uchumi wa wananchi hasa vijana.

Nchimbi amesema katika miaka mitano iliyopita serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania imejiwekeza katika nyanja mbalimbali kama sekta ya afya ,elimu , miundombinu ya barabara za lami mjini na Vijijini kutoka kilomita 39.4 hadi 46.5 pamoja na sekta ya uvuvi.

Akizungumza  leo Septemba 9 ,2025 Nchimbi amesema malengo ya chama cha mapinduzi ni kuboresha maisha ya watanzania na kuwa na taifa lenye kujitegemea.


Pia Nchimbi amezungumzia maendeleo yaliyofanywa na rais Dkt Samia Suluhu Hassan ikiwemo uboreshaji wa bandari ya kasanga ,uwanja wa ndege ,sanjari na kutoa mikopo kwa makundi maalumu.

Balozi Dkt Emmanuel Nchimbi amesema chama kimejipanga kusimamia na kuimarisha huduma za afya kwa akina mama wajawazito na watoto ili kudhibiti na kumaliza vifo vya akina mama wakati wa uzazi kutoka asilimia 9 hadi 4.

Amesema watapunguza udumavu kwa watoto wa chini ya miaka mitanona kuongeza huduma za lishe kwa makundi yanayoathirika zaidi ikiwa ni pamoja na watoto, wajawazito na vijana balehe.


Kwa upande wake Mwenyekiti mstaafu wa chama cha mapinduzi mkoa wa Ruvuma ambaye ameambatana na mgombea mwenza wa urais Hamis Ally amesema chama cha mapinduzi kina mikakati ya kudhibiti ukatili wa kijinsia dhidi ya watoto,wasichana, wanawake,wazee na watu wenye ulemavu.

Sambamba na kuimarisha,makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto pamoja na kuhakikisha mifumo ya malezi inazingatia uwajibikaji na utunzaji wa familia katika Jamii.


Akimkaribisha mgombea mwenza wa urais Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM mkoa wa Rukwa Siraf Maufi amesema wataimarisha huduma za ustawi kwa wazee ikiwamo huduma za afya matunzo na ushirikishwaji katika maamuzi na shughuli mbalimbali za maendeleo.

Nao baadhi ya wananchi na wanachama waliojitokeza kusikiliza sera za chama cha mapinduzi ( CCM) akiwemo Agnes lyoba amesema anawaomba wagombea kutimiza yale   ambayo wanaahidi ili waendelee kuaminika.