Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa CHADEMA, Brenda Rupia amemshukia Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Stephen Wasira, akipinga kauli yake kuwa hakuna kesi za kisiasa nchini.
 
 Akizungumza na wanahabari leo, Jumamosi, Februari 21, 2026, Mkurugenzi huyo amemtaka Wasira kueleza ni jina gani lingine linaweza kupewa kesi ya uhaini inayomkabili Tundu Lissu, ambayo imemfanya akae gerezani kwa siku 319 sasa.
 
 CHADEMA inadai kuwa kesi hiyo imetengenezwa ili kumpa "ahueni" mgombea wa CCM dhidi ya upinzani na kwamba mchakato huo ni matumizi mabaya ya rasilimali za nchi.
 “Wewe kesi kama hiyo wewe unaiitaje? Maana mimi sielewi ukisema hizi kesi sio za kisiasa, hii kesi wewe unaiitaje? Mwenyekiti anakaa gerezani sio kwa kupenda anapotezewa muda, hakuna njia nyingine ya kuisema. 
 
Mnampotezea mwenyekiti muda, mnawapotezea wanachama wa CHADEMA muda kwa kila siku kwenda mahakamani kushuhudia kesi ya uongo”, ameeleza Rupia.