Madiwani wilayani Nkasi mkoani Rukwa wametakiwa kuzingatia maadili ya kazi yao kwa kusoma na kuzingatia sheria ikiwemo kutokuwa sehemu ya chanzo cha migogoro ya ardhi katika jamii.
Hayo yamebainishwa na Kaimu mkuu wa wilaya ya Nkasi ambae pia ni mkuu wa wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa Nyakia Chirukile wakati wa kikao cha kuwajengea uwezo madiwani kuhusu maswala ya maadili na uongozi na kusisitiza kuzingatia usomaji wa sheria za ardhi ikiwemo kuzingatia majukumu ya kazi yao.
Aidha, amewataka kuzingatia maadili kwa kujiepusha na utoaji wa vibari vya ukataji wa miti na kusisitiza kuchukua hatua kali za ksheria na kinidhamu kwa viongozi ambao watabainika kujihusisha na utoaji vibali kinyume na taratibu, kanuni na sheria za nchi.
Afisa tawala mwandamizi Kutoka ofisi ya Tawala za mikoa na Serikali za mitaa (TAMISEM) ndugu Mashaka Makuka amebainisha kuwa lengo la Selikali ni kuwafanya madiwani kuwa na uelewa sahihi juu ya maswala ya uongozi huku kaimu mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Vareliana Mwampasi akisisitiza madiwani kushirikiana na watendaji wa serikali wakati wa utekelezaji wa majukumu yao mahali pa kazi.
Hata hivyo mafunzo yamefanyika kwa muda wa siku mbili yakishirikisha madiwani kutoka kata 28 za wilaya hiyo.

Tunapatikana Kupitia