Aidha, Taarifa kutoka Halmashauri hiyo zimeeleza kuwa kati ya fedha hizo kiasi shilingi1,261,210,000.0 zinatarajiwa kutumika katika ukamilishaji wa ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo huku shilingi1,891,815,000.0 ikiwa ni fedha kwa ajili ya matumizi ya kawaida.
Licha ya hilo, Baraza la madiwani wilayani humo kupitia kikao cha Baraza cha kujadili Rasimu ya mapendekezo ya mpango wa Bajeti kwa mwaka wa fedha 2026/2027 limepitisha mpango wa bajeti ya shilingi 47,396,009,000.00 kati ya hizo shilingi 10,734,616,000.00 ikiwa ni kwa ajili ya miradi ya maendeleo.
Hata hivyo Halmashauri hiyo katika kipindi cha kuanzia Julai 2025 hadi Disemba 2025 kwa mwaka wa fedha 2025/2026 imefanikiwa kukusanya fedha shilingi 2,446,121,275.28 sawa na asilimia 61.95 kati ya lengo la kukusanya kiasi cha shilingi 3,948,818,00.00/=.

Tunapatikana Kupitia