Watu wanne wameripotiwa kupoteza maisha baada ya kusombwa na maji yaliyotokana na mvua kubwa katika Kijiji cha Itekesha, wilayani Kalambo Mkoani Rukwa. Tukio hilo limehusishwa na athari za mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Rukwa na viunga vyake.
Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Mhe Nyakia Ally Chirukile amefika katika eneo la tukio usiku wa tarehe 16 Februari 2026 , Akizungumza na wafiwa na wananchi pamoja na kutoa pole kwa familia zilizopoteza ndugu zao.
Aidha, ameitaka Kamati ya Usalama ya Wilaya kufanya tathmini ya kina ya maeneo hatarishi ili kubaini kiwango cha usalama na kuchukua hatua za haraka.
Pia amewasihi wananchi kuishi katika maeneo salama wakati huu wa mvua na kuepuka kuingilia mikondo ya maji, mabonde na maeneo yenye mkusanyiko wa maji ili kulinda maisha na mali zao

Tunapatikana Kupitia