Watalamu wa Tehama na mawasiliano kwa umma kata ya Mahenje Wilaya mbozi Mkoa wa Songwe  wametakiwa kutumia   utalaamu wao  kama nyenzo ya kuzuia uhalifu katika kata hiyo. 

Rai hiyo imetolewa 10 Februari 2026 na Polisi kata ya Mahenje Mkaguzi wa Polisi Nelson Mwinuka alipo watembelea watalamu hao na kuwambia  kuwa ulinzi jirani ni jukumu la kila mwananchi, hivyo mnatakiwa kufikisha ujumbe sahihi kwa jamii. kwa kuandaa poster, majarida na nyimbo zitakazosaidia kuelimisha jamii dhidi ya vitendo vya uhalifuna wahalifu ili jamii ichukie uhalifu na kata yetu indelee kuwa salama.

Kwa upande wao,watalamu hao waliahidi kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kuhamasisha ulinzi na amani katika kata hiyo ikiwa ni hatua itakayosaidia kujenga jamii yenye mshikamano na mazingira salama kwa wote.