Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma linawashikilia watuhumiwa 22 akiwemo mwanamke mmjo ambao walikuwa wakijihususha na uvunjaji, Uporaji na wizi wa vitu mbalimbali Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma.
Akizungumza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Marco G Chilya amesema mafanikio hayo yamepatikana kutokana na Operesheni Kali zinazoendelea kufanyika Mkoani Ruvuma za kuwasaka na kuwakamata wahalifu wa uvunjaji na Vibaka maarufu kama Vishandu ambao wamekuwa wakijihususha na Uporaji wa mikoba yakina mama nyakati za usiku wakitumia Pikipiki zisizokuwa na namba za usajili

Vilevile kupitia Operesheni hizo pia Jeshi Polisi Mkoa wa Ruvuma limefanikiwa kukamata  Pombe Moshi (Gongo) jumla ya lita 58, Pikipiki 22 zilizokuwa zikitumika katika Uporaji maeneo mbalimbali ya Manispaa ya Songea, Televisheni 9 na Redio aina ya Subwoofer 8 ambapo kati ya Mali hizo Televisheni 4 na Redio 2 zimelitambulika na kukabidhiwa kwa wahusika.

Operesheni hizo ni endelevu Mkoani Ruvuma hivyo watu wote wanaojihusiha na vitendo vya uhalifu waache mara Moja kwani Mkoa wa Ruvuma sio salama kwao badala yake watafute shughuli zingine zakuwaingizia kipato halali"Alisema Kamanda Chilya - SACP"

Sambana na hilo alimalizia kwa kuwakumbusha Wananchi wote Mkoa wa Ruvuma hasa wanawake kuacha tabia za kuzurula nyaki za usiku pasipo sababu za Msingi sanjari na kuwasihi kutopanda Bodaboda ambazo hazina namba za usajili kwani madereva hao hutumia mwanya huo kutekeleza uhalifu kwa kuwapora mali zao